Mikopo kwa wanawake jasiri nchini Tanzania

Grace Patrick Kimaro ni Mwanamke Jasiri.

Ni mjasiriamali wa kitanzania mwenye maduka saba ya vifaa vya simu, na miongoni mwa bidhaa anazouza ni pamoja na chaja cha simu, nyaya,  na vikasha vya kukinga simu. Haya yote ameweza kuyafanya kutokana na  dhamana za kijinsia za benki ya NMB zilizotolewa mwaka 2022. Ameweza kukuza biashara yake na hadi sasa ameweza kuajiri watu 19. 

“Grace ni miongoni mwa wateja wetu na mnufaika wa huduma zetu mbalimbali tunazotoa ambazo tunaita wanawake jasiri kutokana na kuwepo kwa sifa ya ujasiri, tukiwa na maana ya ‘mwanamke anayeweza kuendesha biashara yake mwenyewe na kupata mafanikio…anakuwa na simulizi la mafanikio kwenye jamii’, anaeleza Alex Mgeni, Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, Tanzania.

Dhamana za NMB zinazoitwa Jasiri — ni dhamana za kwanza ya kijinsia kusini mwa jangwa la Sahara – inawakilisha eneo jipya na linalokua la huduma za kifedha kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa fedha kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake. Inasaidia pia utekelezaji wa mpango mpana wa serikali ya Tanzania kwa kuleta usawa na kuongeza idadi ya wanawake kwenye sekta binafsi.  

Kimaro, ni mama wa watoto wanne ambaye ndoto zake za kibiashara zilikwamishwa na ukosefu wa mtaji wa kutosha, hatifungani hii imekuwa mkombozi. Nchini Tanzania, asilimia 75 ya biashara zinazomilikiwa na wanawake zinakosa mtaji wa kuziendeleza.

“Mkopo kutoka NMB umenisaidia kukua kibiashara,” alieleza akiwa dukani kwake jijini  Dar es Salaam. “Nimepata mafanikio mengi na nimeweza kuwalipia wanangu kutokana na kuendesha biashara yangu mwenyewe.”
Grace Patrick Kimaro, Mjasiriamali wa Tanzania

Kwa nini hatifungani vya jinsia?

Hatifungani za Jinsia zimebuniwa  kwa ajili ya kukuza, kuwezesha na kuleta usawa katika biashara zinazomilikiwana wanawake. Mpango huu wa mikopo kupitia hatifungani hizi lazima uende sambamba na malengo haya.  

Tangu 2013, takribani dhamana za kijinsia 80 zimetolewa duniani kote zinazoendana na  Kanuni za Dhamana za Kijamii au Kanuni Endelevu za Dhamana, na taasisi zaidi zinachukulia mikopo kama chanzo cha kupata fedha za kuendeleza usawa wa kijinsia.

“Wanawake wanapopata mikopo na nyenzo za kukuza biashara, wanakuwa injini madhubuti za kukuza uchumi, kutengeneza ajira na uvumbuzi."
Mary Porter Peschka, Mkurugenzi wa IFC Kanda ya Afrika Mashariki

IFC, ni kitengo cha Benki ya Dunia cha kuhudumia sekta binafsi, ilichangia asilimia 31 ya dhamana za benki ya NMB, sawa na takribani dola milioni kumi. Uwekezaji wa IFC kwenye dhamana unatokana na ufadhili wa mfuko wa mikopo kwa fedha za ndani wa International Development Association's (IDA) Private Sector Window.

Alex Mgeni, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Biashara wa Benki ya NMB.

Alex Mgeni, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Biashara wa Benki ya NMB.

Dhamana za kijinsia za benki ya NMB zitawanufaisha zaidi ya kampuni ndogo na za kati 2,000 zinazomilikiwa na wanawake nchini Tanzania, kama ambavyo Kimaro alivyonufaika, kwa kupata mikopo ya kati ya TZS milioni moja hadi TZS bilioni 4.5, au kati ya dola za kimarekani 400 hadi milioni 1.8.

Muonekano kutoka wa duka la Kimaro.

Muonekano kutoka wa duka la Kimaro.

Kuziba mapengo ya kijinsia

Uwekezaji wa IFC kwenye benki ya NMB kupitia dhamana za kijinsia ni sehemu ya majukumu yake mapana ndani ya Tanzania kwa kusaidia kuondoa mapengo ya kijinsia na kupigania wanawake kwenye sekta binafsi.  

Mbali na kusaidia dhamana za kijinsia za benki ya NMB, IFC ilizindua mpango wake wa Anaweza: She Can mwezi Juni, 2023 unaolenga kufanya kazi na washirika wake kwa ajili ya kuongeza idadi ya wanawake kwenye sekta binafsi. Mpango wa ‘She Can’ utaendeleza mafanikio ya mpango mwingine wa IFC wa  ‘Finance2Equal’ ulioshirikisha sekta ya fedha kwa ajili ya kuongeza idadi ya wanawake viongozi kwenye sekta ya fedha nchini Tanzania.

Kimaro akifanya shughuli ya simu kwenye duka lake.

Kimaro akifanya shughuli ya simu kwenye duka lake.

Iliyochapishwa mnamo Oktoba 2023